Wamiliki wa Klabu ya Manchester United, Familia ya Glazer wamesema wanafikiria kuuza Klabu hiyo ya England, huku wakiendelea kusaka mbinu mbadala.

Familia hiyo kutoka nchini Marekani waliinunua Klabu ya Manchester United mwaka 2005 kwa thamani ya Pauni Milioni 790 sawa na Dola za Marekani Bilioni 1.34, kwa wakati huo.

Maamuzi ya kutangaza wanafikiria kuiuza klabu hiyo yenye Maskani yake Makuu Old Trafford, yemekuba baada ya Maandamano kadhaa kufanywa na baadhi ya Mashabiki na Wanachama ambao walionyesha kuchukizwa na MPango wa uendeshaji kutoka kwenye Familia hiyo.

Taarifa kutoka Klabuni hapo zinaeleza kuwa Bodi itazingatia njia zote mbadala za kimkakati, ikiwa ni pamoja na uwekezaji mpya katika klabu, mauzo, au miamala mingine inayohusisha Kampuni.

Imeongeza kuwa mchakato huo utajumuisha tathmini ya mipango kadhaa ya kuimarisha klabu, ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa Uwanja, Miundombinu na upanuzi wa shughuli za Kibiashara za kilabu katika kiwango cha kimataifa, ili kuongeza mafanikio ya muda mrefu ya klabu hiyo kwa upande wa Timu za Wanaume, Wanawake na Vijana ili kuleta manufaa kwa Mashabiki na Wanachama wengine.

“Tunapotafuta kuendelea kujenga historia ya mafanikio ya klabu, bodi imeidhinisha tathmini ya kina ya njia mbadala za kimkakati,” wamesema wanafamilia Avram Glazer na Joel Glazer.

“Tutatathmini chaguzi zote ili kuhakikisha kuwa tunawatumikia vyema Mashabiki wetu na kwamba Manchester United inaongeza fursa kubwa za ukuaji zinazopatikana kwa Klabu leo ​​na katika siku zijazo.”

“Katika mchakato huu tutaendelea kulenga kikamilifu katika kutumikia maslahi ya Mashabiki wetu, Wanahisa na Wadau mbalimbali.”

Mwaka 2012, Familia ya Glazers iliuza Asilimia 10 ya hisa zake kupitia orodha ya hisa na waliendelea kufanya hivyo katika miaka iliyofuata.

Familia ya Glazer pia inamiliki timu ya inayoshiriki Mchezo wa American Footbal ‘NFL’ ya Tampa Bay Buccaneers tangu mwaka 1995 na Avram Glazer alinunua timu katika ligi mpya ya kriketi ya Falme za Kiarabu ya Twenty20 mnamo 2021.

Joel na Avram walichukua nafasi ya kuiendesha Mancheser United katika shughuli za kila siku, baada ya baba yao Malcolm kuugua kiharusi Aprili 2006. Bilionea Malcolm alifariki akiwa na umri wa miaka 85 mwaka wa 2014.

Kampuni ya uwekezaji ya Marekani ya Raine Group, ambayo ilishughulikia mauzo ya Chelsea ya £4.25bn mwezi Mei, inakaimu kama mshauri wa kipekee wa masuala ya kifedha wa United.

Taarifa kutoka Mancheser United iliongeza: “Hatuwezi kuwa na uhakika kwamba uhakiki unaofanywa utasababisha shughuli yoyote inayohusisha kampuni.”

“Manchester United haina nia ya kutoa matangazo zaidi kuhusu mapitio isipokuwa, bodi iwe imeidhinisha shughuli maalum au hatua nyingine inayohitaji tangazo rasmi.”

United, ambayo inashika nafasi ya tano kwenye Msiammo wa Ligi Kuu ya England, haijashinda Ubingwa wa Ligi hiyo tangu mwaka 2013 na haijashinda taji lolote tangu ilipotwaa ubingwa wa Europa League na Kombe la EFL mnamo 2017.

Kumekuwa na maandamano mengi dhidi ya umiliki wa Glazers katika miaka ya hivi karibuni, likiwemo zoezi la mwezi Mei Mwaka 2021, ambalo lilisababisha mchezo wa Ligi Kuu kati ya United dhidi ya Liverpool kuahirishwa.

Maelfu ya wafuasi waliandamana hadi kwenye Old Trafford wakipinga kabla ya mechi hiyo hiyo msimu huu, mwezi Agosti.

United walikuwa sehemu ya mradi wa Ligi Kuu ya Ulaya uliofeli ambao uliporomoka haraka Aprili 2021. Mwenyekiti mwenza wa Manchester United Joel Glazer baadaye aliomba radhi kwa machafuko yaliyosababishwa.

Tangu wakati huo amehudhuria vikao vya mashabiki kufuatia ghasia za wafuasi wake na kuahidi kutoa hisa kwa wafuasi wa klabu hiyo.

Kulingana na Transfermarkt, United wametumia jumla ya euro Bilioni 1.36 sawa na Pauni Bilioni 1.18 kwa usajili wa Wachezaji chini ya Glazers, na Manchester City pekee ndio ilikua klabu pekee iliyotumia pesa nyingi katika kufanysa usajili kwa kipindi hicho.

Hatua ya kuuzwa kwa United imekuja baada ya mwenyekiti wa Liverpool, Tom Werner kusema kuwa Fenway Sports Group “inachunguza mauzo” ya klabu hiyo ya Anfield.

Ripoti ya Bloomberg mnamo Agosti 2022 ilisema familia ya Glazer ilikuwa tayari kuuza hisa za wachache katika klabu.

Bilionea wa Uingereza Sir Jim Ratcliffe alisema angependa kuinunua United kabla ya mwezi Oktoba, lakini Familia ya Glazer ilimwambia hawataki kuiuza.

Mashuhuda ajali ya Daladala Mbezi 'wafunguka'
Manchester United, Ronaldo wapigana vijembe