Klabu ya Manchester United imetwaa ubingwa wa kombe la Europa mara baada ya kuichapa timu ya Ajax Amsterdam magoli 2-0 huku ikijihakikishia kucheza michuano ya vilabu bingwa barani ulaya kwa msimu ujao.

Aidha, magoli ya Manchester yalifungwa na Paul Pogba na Hendrick Mkhtaryan katika fainali iliyofanyika mjini Stockholm nchini Sweeden, ambapo katika mchezo huo Manchester ilicheza kwa ushirikiano mkubwa.

Mapema kabla ya mchezo huo kuanza, timu hizo mbili zilitoa heshima zao kwa watu waliopoteza maisha katika shambulio la kigaidi mjini Manchester. Pia wachezaji wa Manchester United walivaa vitambaa vyeusi mikononi kama ishara ya heshima kwa waathirika

Wakicheza bila ya mfungaji bora wao Zlatan Ibrahimovic, pamoja na mabeki Marcos Rojo, Luke Shaw, pamoja na Erick Bailly anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu, kikosi cha Mourinho kililazimika kujituma kwenye mchezo huo wa 64 msimu huu.

Wakitumia uzoefu, pamoja na jinsi walivyojipanga, waliweza kukisumbua kikosi cha Ajax ambacho kilikuwa na wachezaji chipukizi, wakiwa na wastani wa umri wa miaka 22

Manchester United sasa wanaungana na Chelsea, Tottenahm na Manchester City katika kucheza Klabu Bingwa Ulaya. Pia ushindi huu utawaingizia kitita cha takriban pauni milioni 50.

 

Magazeti ya Tanzania leo Mei 25, 2017
Trump apingwa vikali Ubelgiji, wananchi waandamana