Meneja wa Klabu ya Manchester United, Erik ten Hag ametwaa tuzo ya Kocha bora wa mwezi Septemba zinazoandaliwa na Ligi Kuu England, Marcus Rashford akichukua tuzo ya mchezaji bora.

Ten Hag alianza msimu vibaya kwa kupokea vichapo viwili mfululizo dhidi ya Brigton iliyoichapa Man United mabao 2-1, Brentford ikitoa kipigo cha kushtukiza cha mabao 4-0.

Hata hivyo Ten Hag akarudi kwa kishindo na kugawa dozi katika mechi nne mfululizo za Ligi Kuu England, Man United ilipocheza dhidi ya Southampton, Liverpool, Leicester City na Arsenal.

Mholanzi huyo anakuwa kocha wa pili kubeba tuzo hiyo tangu Ole Gunnar Solskjaer alipoibeba mwaka 2019 kabla ya kufungashiwa virago Novemba, mwaka jana.

Kwa Upande wa Rashford alionyesha kiwango safi kwenye mechi mbili alizocheza dhidi ya Leicester na Arsenal. Rashford alitoa asisti mbili na kufunga mabao mawili.

Ten Hag atakiongoza kikosi chake kuwakabili mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Manchester City utakaochezwa Etihad, siku ya Jumapili.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Octobar 1, 2022
Ally Kamwe: Tunakwenda kuandika historia mpya