Klabu ya soka ya Manchester United imetinga hatua ya fainali ya Kombe la FA baada ya kuifunga Tottenham Hotspur mabao 2-1, kwenye mchezo wa nusu fainali.

Spurs ndio walikuwa wa kwanza kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 11 kupitia kwa kiungo Delle Ali kabla ya mshambuliaji Alexis Sanchez kusawazisha bao hilo dakika ya 24 na kufanya kipindi cha kwanza kimalizike kwa sare.

Aidha, Kipindi cha pili Manchester United walijihakikishia kucheza fainali baada ya kiungo wa Kihispania Ander Herera kufunga bao la pili dakika ya 62 na kuzima ndoto za Tottenham za kusaka walau taji moja baada ya kuwa na kikosi bora kwa misimu kadhaa.

Hata hivyo, Man United sasa inasubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Chelsea inayofundishwa na Conte ambayo itacheza na Southampton inayofundishwa na Mark Hughes nusu fainali hiyo itapigwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Makala: Vyakula vitakavyokuza nywele zako haraka na kuzipa afya
Idris 'ala shavu' Uber

Comments

comments