Kiungo mshambuliaji kutoka nchini England Jadon Malik Sancho, bado anaendelea kuwashughulisha Manchester United ambao wana dhamira ya kumsajili katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.

Manchester United waliwahi kuonyesha dhamira ya dhati ya kumsajili kiungo huyo wa klabu ya Borussia Dortmund, lakini walirudi nyuma baada ya kutajiwa ada yake ya usajili, kwa kudai ni kubwa.

Uongozi wa Borussia  Dortmund umetangaza ada ya usajili ya Pauni milioni 108, kwa mchezaji huyo, na mpango wa Manchester United wa kutaka kurudi kwenye harakati za kumsajili Sancho unadhihirisha huenda wakakubaliana na kiasi hicho cha pesa.

Manchester United wamedaiwa kujifungia kwenye mazungumzo na mawakala wa Sancho kwa sasa wakijadili kuhusu mshahara pamoja na ada za kamisheni kwa madalali hao kabla ya kwenda kwa mabosi wa Dortmund kumalizana juu ya mpango wa ada.

Mtaalamu wa masuala ya uhamisho wa wachezaji, Dharmesh Sheth aliiambia Sky Sports News: “Kama utawasikiliza Dortmund wanachosema utaona dili hilo halipo. Lakini halijafa bado.”

TRA kupita mlango kwa mlango
Shiboub kucheza Ligi kuu Algeria