Meneja wa klabu ya Inter Milan, Roberto Mancini amesema kufungwa katika mchezo wa ligi dhidi ya Fiorentina, hakujabadilisha lolote katika harakati zake za kuiwezesha klabu hiyo ya mjini Milan kufanya vyema msimu huu.

Mancini, amesema kufungwa mabao manne kwa moja katika mchezo huo, amekuchukulia kama changamoto ya kujipanga vyema kwa kuamini hakuna litakaloshindikana kwa msimu huu kufanya jambo alilolikusudia.

Amesema pamoja na kutofurahishwa na matokeo hayo ambayo hakuyategemea, bado kikosi cha Inter Muilan kinaendelea kuwa na nafasi nzuri ya kupambana kwenye harakati za kuendelea kukaa kileleni ambapo kwa sasa wamezidiwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya Fiorentina ambao wanashika nafasi ya kwanza.

Hata hivyo meneja huyo ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Man city na kukipa ubingwa mara mbili wa nchini England, amesisitiza wachezaji wake walicheza soka safi usiku wa kuamkia hii leo, lakini bahati ya kutumbukiza mpira katika nyavu za Fiorentina haikua kwao.

Pamoja na kukiri hivyo Mancini hakusita kuwapongeza wapinzani wake Fiorentina kwa kusema ushindi walioupata ulistahili kutokana na makossa ya kikosi chake ambayo yalikua yakijitokeza mara kwa mara.

Ushindi wa mabao manne kwa moja umeiwezesha Fiorentina kufikisha point 15, sawa na Inter Milan na sasa wapo kileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

24 Waitwa Kuivaa Malawi
Arsene Wenger Ampotezea Jose Mourinho