Meneja wa klabu ya Inter Milan, Roberto Mancini ameonyesha kuwa tayari kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya England.

Magazeti ya The Daily Mirror pamoja na The Express mapema hii leo yametoka na taarifa zinazomuhusu meneja huyo, ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Man city na kufanikiwa kufuta utejwa wa kukosa mataji kwa kipindi cha zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Mancini mwenye umri wa miaka 51, amenukuliwa na vyombo hivyo habari akisema kwamba, anaamini ana uwezo wa kutosha wa kukiongoza kikosi cha England na kufanikisha azma ya kufanya vyema katika medani ya kimataifa.

Alisema ni wazi hana budi kuingia katika mpango wa kuwania nafasi hiyo, kutokana na viongozi wa chama cha soka nchini England (FA) kutoa nafasi ya upendeleo kwa makocha wa kigeni pindi mckato utakapoanza.

England kwa sasa hawana kocha mkuu wa timu ya taifa, kufuatia Roy Hodgson kutangaza kujiuzulu siku moja baada ya timu yake kuondolewa kwenye fainali za Euro 2016, kwa kufungwa na Iceland mabao mawili kwa moja.

Arsenal Waonyesha Dhamira Ya kweli Kwa Alvaro Morata
Chelsea Wajitosa Kwa Kalidou Koulibaly