Ikiwa imesalia miezi 9, siku 279 mwaka kuisha, ifahamike kuwa kipimo cha maisha ya binadamu ni mafanikio.

Ujumbe wa leo unasema,

”Mafanikio yana uhusiano mkubwa na matendo, mtu mwenye mafanikio husonga mbele, haijalishi ni mara ngapi anakosea kikubwa hakati tamaa na kuyachukulia makosa kama sehemu ya maisha ya kujifunza kitu kipya”.

Watu wengi huogopa, na hukasirika pindi wanapokosolewa, huvunjika moyo , hujihisi wanyonge na hujiona hawawezi  pia.

Ukweli ni kwamba watu matajiri duniani wamepitia changamoto kada wa kada, ikiwemo kukosolewa na kuambiwa huwajui, lakini changamoto hizo wakazigeuza kuwa fursa ndio maana wamefikia hapo walipo sasa.

Kikubwa katika maisha kujitambua, umetoka wapi, upo wapi na unaenda wapi, huo ndio ufunguo wa maisha mbali na hilo utakuwa ni mtu wa kuyumba yumba daima.

Heshimu mawazo ya mtu, kuwa mnyenyekevu, jishushe, jiheshimu utaheshimika, usiwe mjuaji, fikiri kabla ya kutenda, usichopenda kufanyiwa usimfanyie mwenzako, haya ni maisha, hakuna aijuaye kesho yake, la mwisho usimdharau usiyemjua.

Dar24 Inawatakia siku njema, yenye mafanikio tele, hata maandiko yanasema asiyefanya kazi na asile, kazi njema Watanzania katika kujenga taifa letu.

 

Kamanda aahidi ukilema kwa watakaoandamana Aprili 26
Putin aipa kisogo mahakama ya kimataifa, kumneemesha Bashir