Msanii wa Bongo Flava, Rayvanny kutoka Wasafi Classic Baby (WCB) ameshinda tuzo ya BET (Black Entertainment Television) kipengele cha ‘Viewers Choice Best New International Act Artist’.

Kufuatia ushindi huo msanii Diamond Platnumz ambaye anaiongoza WCB amepongeza ushindi huo wa Rayvanny, amesema kuwa zaidi ya miaka mitatu tunaenda na kurudi patupu lakini safari hii si patupu tena kufuatia ushindi huo.

“Hatimaye leo Unakuja nayo Tanzania Dah! ….Zaidi ya miaka mi 3 tunaenda na kurudi Patupu….Hakika Maisha Uvumilivu na kutokata tamaa…. BRING IT HOME BOSS!!! @babutale”

“WOOOOOOOOOYOOOOOOOO!!!!!!!….. Nikishindwa kwa Mkono wa Kulia, ntatumia hata Mkono wa Kushoto…..ila lazma ifike @Wcb_Wasafi TANZANIA!!!! Chkua hiyo #Wcb_Wasafi #WinningTeam!”

Lori lalipuka na kuteketeza watu 123, Pakistan
Video: Manji akubali yaishe kwa JPM, Lowassa ataka mkakati kukabili kamatakamata