Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, Masista wa Maria Consolata na wote walioguswa na kifo cha mabinti mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti waliofariki dunia usiku wa Juni 2, 2018 katika hospitali ya Mkoa wa Iringa.

Rais Magufuliwa aliwatembelea Maria na Consolata walipokuwa wakipata matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam January 6, 2018, ambapo pia aliwaliongoza sala ya kuliombea Taifa na Viongozi wake.

Rais Magufuli anasema anatambua kuwa Maria na Consolata walikuwa na ndoto kubwa ya kuja kulitumikia Taifa baada ya kumaliza Chuo Kikuu cha Masista Ruaha (RUCO) walikokuwa wakiendelea na masomo yao, lakini haikuwa hivyo.

Maria na Consolata walikuwa watoto yatima, na walikuwa wakilelewa na kusomeshwa na Masista wa Kanisa Katoliki.

Safari ya Maria na Consolata imetuachia funzo kubwa sana
Video: Ofisa alipwa mshahara mara 10 zaidi ya JPM, Ngeleja, Kalamagi, Yona watajwa tena