Kufuatia mdogo wake Mange Kimambi kufika Ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kusuluhisha mgogoro wake wa kutelekeza mtoto Mange amesema kuwa hajafurahishwa na kitendo hicho.

Amesema kuwa amechukizwa na kitendo hicho cha mdogo wake kufika ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, ambapo ameandika kwenye ukurasa wake Instagram ataifufua kesi ya mirathi iliyoamuliwa mwaka 2016.

Aidha, katika hatua nyingine Mange ameituhumu familia yake kwa kuuza machimbo ya urithi ya kokoto kwa bei ndogo yaliyopo Tegeta jijini Dar es salaam bila kupewa taarifa wala kutumiwa mgao wake.

“Nilikuwa tayari niishi vibaya ila nyinyi muishi vizuri ndio maana sikuwasumbua na mali za baba yetu, Mgao wangu wa machimbo ya kokoto mliyouza muanze kunitafutia. Mlidhani sijui? Kweli mnadhani sijapewa habari za nyinyi kuuza machimbo yetu ya kokoto? Nilikuwa najua Ila niliamuwa kukaa kimya sababu nawapenda na bila nyinyi kwenye maisha yangu nahisigi siwezi kuishi ila labda nahitaji kujifunza kuishi bila nyinyi,”ameandika Mange kwenye ukurasa wake wa Instagram

Hata hivyo, amesema kuwa mpaka sasa hajachukua chake kwani hadi leo ni miaka 12 sasa imepita tangu jaji awagawanye mali za urithi

Zari amtukana Diamond, amkumbusha kuhusu watoto 
Mkurugenzi Halmashauri ya Kongwa afariki dunia

Comments

comments