Uongozi wa klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC umetoa taarifa za kukamilisha maandalizio ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya mtoano dhidi ya Red Arrows kutoka Zambia.

Simba SC itakua mwenyeji katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam siku ya Jumapili (Novemba 28), huku mchezo wa Mkondo wapili ukitarajiwa kuchezwa Desemba 5.

Mwenyekiti wa Simba SC Murtanza Mangungu amesema upande wa Uongozi wamekamilisha utaratibu wa maandalizi kuelekea mcheza mchezo huo, huku wakiamini ushindi utapatikana siku ya Jumapili.

Amesema Uongozi umefanya kila kitu kinachohitajika upande wa timu na maandalizi mengine ambayo ni maagizo kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’.

Mangungu amesema upande wa kikosi chao, Kocha Pablo anaendelea na maandalizi jijini Dar es salaam na amewahakikishia kila kitu kitakua vizuri kutokana na Program anazozitumia kwenye mazoezi.

“Kwa sasa Kocha anaendelea kuwapa mbinu wachezaji na nina amini kwamba kwa umuhimu wa mashindano ya kimataifa tutafanya vizuri na kupata matokeo.”

“Ushindani ni mkubwa kwa kuwa kila timu ipo wazi ni imara na zina ubora hilo halitupi mashaka kwani wachezaji wetu tulionao ni imara na wana uzoefu kimataifa.” amesema Mangungu.

Simba SC iliangukia kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa Ligi Mabingwa Barani Afrika kwa kufungwa na Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Amri Kiemba: Kuna tatizo kubwa Azam FC
Pablo afurahia kikosi Simba SC