Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa ameitaka Manispaa ya Ilala kuharakisha kuunda kamati ili kurahisisha utendaji kazi kutoka katika ngazi za mitaa na Wilaya.

Ameyasema hayo alipokutana na walemavu Wilayani Ilala akiwa katika ziara yake ya kukutana na walemavu ambapo amesema kuwa Ilala bado ikonyuma katika kuunda kamati hizo kwani mpaka sasa imeunda kamati 27 kati ya kata 36 na mitaa 76 kati ya mitaa 156.

“Fanyeni juhudi kubwa katika kuunda hizi kamati zina umuhimu mkubwa zitasaidia kuanzia huko chini kupata takwimu na siyo tu kwamba ziundwe bali zifanye kazi,“amesema Ikupa

Aidha, ameikumbusha Manispaa hiyo kutoa mafuta chupa moja kila baada ya miezi mitatu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ‘Ualbino’ na kuagiza mikopo ya asilimia mbili kwa walemavu iendelee kutolewa kwa utaratibu uliowekwa badala ya kupewa kikundi fulani ili kiwagawie wengine.

‘’Tayari tumesha weka kanuni za utoaji mikopo hili, suala la kusema kipewe kikundi fulani haliwezekani mimi ni mkweli nakwa wale mliochukua mikopo ya Bajaji mlitaka mpunguziwe rejesho nimezungumza na mkurugenzi amesema inawezekana mtakutana naye ili mliweke sawa,’’ameongeza Ikupa

Pia ametoa rai kwa mkoa wa Dar es salaam ,kuviunga mkono vikundi vya wenye ulemavu wanao tengeneza vifaa saidizi badala ya kuendelea kununua kutoka nje na kusema kuwa hata Rais Magufuli anasisitiza watanzania wapende vya kwao ili kuendeleza viwanda vya ndani.

Pamoja na hayo Naibu huyo, amewapongeza watu wenye ulemavu kwa kuendelea kuwa watulivu na kusema kuwa matatizo na malalamiko yao kuhusu kuvamiwa na watu wengine katika sehemu zao za kazi ya kuendesha bajaji zitafanyiwa kazi na Manispaa na kusema kuwa itafanika operesheni kubwa ya kuwaondoa watu wanao fanya kazi hizo katika maeneo ya walemavu bila utaratibu.

Kwa upande wao watu wenyeulemavu walio pata fursa ya kuzungumza katika  mkutano huo  pamoja na kumpongeza Naibu waziri , wamempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kuwajali walemavu  na kuwapatia mikopo ya asilimia mbili , kuwawekea waziri anaye shughulikia masuala yao  jambo ambalo limewafanya kujisikia nao kama binadamu wengine.

 

Zanzibar: Hofu yatanda, Watu nane wapotea na Boti Baharini
Bondia afariki baada ya pambano