Manispaa ya Ubungo imepanga kuwakusanya na kuwasikiliza watoto wanaolala katika daraja la Kijazi lililopo mkoani Dar es Salaam ili waweze kuzungumza nao na kufahamu mambo yaliyowafanya watoke majumbani kwao na kuanza kuishi mtaani.

Hayo yamebainishwa na Meya wa Manispaa ya Ubungo, Jaffari Juma Nyaigesha ambaye amesema lengo la kufanya hivyo ni  ni kutaka kuwaweka katika mazingira salama kwani kuwarudisha makwao bila kufahamu mazingira wanayorudishwa kunaweza kuwafanya kurejee mitaani.

“Tumekubaliana mimi  na wenzangu, tukusanye wale vijana, tukae nao tuongee, tuweze kusikiliza nini shida iliyowatoa makwao na kuna tatizo gani, kwa sababu unaweza kusema unambeba unamrudisha makwao, hali ikawa ni ileile,” amesema Nyaigesha.

Huyu ndiye mrithi wa Fatou mahakama ya ICC
Balozi Mulamula aomba radhi