Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans, Yusuf Manji amemeendelea kupongezwa na kusifiwa kwa kuchaguliwa tena kuiongoza klabu hiyo bila kupingwa katika uchaguzi uliofanyika Juni 11,2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

Jana, Chama cha soka mkoa wa Dar e salaam (DRFA) kiliongeza pongezi hizo kwa mwenyekiti huyo na kumtakia utendaji uliotukuka.

Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kasongo alisema kuwa kitendo cha Manji kupata kura nyingi ni ishara tosha kwamba anakubalika na wanachama wa klabu hiyo licha ya kuwa hakuwa na mpinzani kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya mwenyekiti.

Kasongo pia alimpongeza Clement Sanga kwa kurudi tena kwenye nafasi ya umakamu mwenyekiti kupitia uchaguzi huo.

Aidha, Kasongo amemuhakikishia Yusuph Manji  kuwa DRFA itaendeleza ushirikiano uliopo na uongozi wake pamoja na kamati nzima ya utendaji ya Yanga katika masuala mbalimbali ya kuendeleza soka la Dar es salaam.

Jana, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi pia alimpongeza Manji kwa ushindi alioupata na kuanza muhula mpya katika kiti hicho ndani ya klabu hiyo.

Manji aliweza kuitetea nafasi ya Uenyekiti kwa kupigiwa kura 1,468 kati ya kura zote 1,470 zilizopigwa licha ya uchaguzi huo kutanguliwa na mizengwe ya mbio za vikwazo zilizoishia sakafuni.

Tarehe ya Yanga kukabidhiwa 'Chao' na Vodacom yawekwa wazi
Video: Chris Brown, Wizkid wafunika jukwaani na wimbo wao mpya