Bingwa wa zamani wa ngumi duniani ambaye hivi sasa ni Seneta nchini Ufilipino,Manny Pacquiao amekanusha taarifa zilizokuwa zikiripotiwa na vyombo vya habari zikimnukuu promota wake kuwa ameamua kurudi tena ulingoni ikiwa ni miezi michache baada ya kutangaza kustaafu.

Awali, vyombo vya habari vilimnukuu promota wake, Bob Arum akieleza kuwa Manny Pacquiao ameamua kuomba likizo ya kutohudhuria vikao vya Bunge la Ufilipino kwa muda ili ajifue na kupambana na bondia mmoja machachari mwaka huu. Wengi wakimtaja Canelo Alvarez wa Urusi.

Manny-Pacquiao

Kupitia Instagram, Manny Pacquiao ameweka tamko rasmi linalotoka katika ofisi yake akieleza kuwa hana mpango wa kufanya hivyo na kwamba kipaumbele chake ni kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi hivi sasa.

Amesema kuwa alipokuwa anafanya kampeni aliwahakikishia wananchi wake kuwa atahudhuria vikao vyote vya Bunge na kwamba anataka kuhakikisha anatimiza ndoto hiyo hivyo hana mpango wa kuomba likizo.

“Kama itatokea ninataka kupigana tena ulingoni, nawahakikishia, itafanyika wakati hakuna Bunge kwahiyo hakutakuwa na haja ya kuomba likizo. Mazoezi yote nitakayoyafanya nitafanyia hapa Ufilipino ili kuhakikisha nahudhuria vikao vya Bunge wakati nikiwa naendelea na mazoezi, ameandika Manny Pacquiao.

“Ndondi kwangu ndio chanzo pekee cha kuendesha maisha yangu na familia na kuwasaidia watu walio na mahitaji. Siasa kwangu ni kama chuo cha mafunzo na sio chanzo cha kuendesha maisha yangu,” aliongeza.

Henry Joseph Awaombea Kila La Kheri Walioondoka Mtibwa Sugar
Shirika La Ndege La Kenya Kuwaleta Wapinzania Wa Young Africans