Bondia Mfilipino, Manny Pacquiao amempiga Mmarekani Timothy Brandley katika pambano lao la tatu lililofanyika leo alfajiri katika ukumbi wa MMG, Grande Arena, Las Vegas nchini Marekani.

Majaji watatu wa pambano hilo wote walimpa Manny Pacquiao ushindi wa  116-110, hivyo kuwa Bingwa mpya wa Dunia wa uzito wa ‘Welterweight’ wa WBO.

Pacquiao 1

Manny alimuangusha chini Brandley mara mbili katika pambano hilo, ikiwa ni katika raundi ya 7 na raundi ya 9.

Akizungumza baada ya pambano hilo, Pacquiao alikiri kuwa anaastafu masumbwi na sasa ataendelea na shughuli zake za kuwatumikia wananchi wa Ufilipino akiwa kama Mbunge wao.

“Ndio nastaafu,” alisema. “Nataka kwenda nyumbani kwa familia yangu na kuwatumikia watu wangu. Nawapenda mashabiki wangu na nawashukuru kwa ‘sapoti’ waliyonipa,” aliongeza.

Manny Pacquiao na Brandley 2

Hili lilikuwa pambano la tatu kati yao, ambapo mara ya kwanza walipigana mwaka 2012 na Brandle alitangazwa mshindi lakini ushindi wake ulizua utata na sehemu kubwa ya wahudhuriaji ilisikika ikipinga kwa kuzomea. Alipouliza Brandley kama anaamini alishinda, alidai kuwa angeomba akaangalie tena pambano lao kwenye ‘mkanda’ ndipo ataweza kueleza kama alishinda. Pacquiao alidai kuwa anaamini alishinda.

Wawili hao walirudi ulingoni mwaka 2014 na Pacquiao alitangazwa kuwa mshindi huku Brandley akikiri kupoteza pambano hilo.

Wabunge warudia maswali ya Lowassa kuhusu Uamuzi wa Magufuli kwenye fedha
Waarabu Walazimisha Sare Dar es salaam