Bondia wa Ufilipino, Manny Pacquiao ambaye pia ni Seneta nchini kwao, ameweka wazi kuwa pambano lake lijalo litafanyika Juni 24 mwaka huu jijini Kuala Lumpur, Malaysia.

Pacquiao ambaye alipotezea pambano la marudiano na bondia wa Australia, Jeff Horn amesema kuwa atapanda ndege kwenda Malaysia kuzichapa na bondia machachari, Lucas Matthysse ambaye ni raia wa Argentina.

“Tumeshafikia makubaliano, nitapigana nchini Malaysia, Juni 24 dhidi ya Matthysse. Nitakuwa nimemaliza maandalizi yatakayochukua wiki 11,” Pacquiao aliiambia Manila Times.

Promota wake, Bob Arum amesema kuwa wamekuwa wakizitafuta fedha za Mashariki ya Kati na sasa wamepata za Mashariki ya Mbali hivyo kwao ni jambo la furaha. Amesema kuwa Pacquiao anatarajia kuingiza $15 milioni kwa pambano hilo.

Matthysse ni bondia nguli na machachari mwenye rekodi ya kushinda mapambano 39 (36 kwa KO) kati ya mapambano 43, akishindwa mapambano 4.

Rais Xi Jinping wa China kutawala maisha
Mkakati mzito wa kumng'oa Lissu TLS wasukwa

Comments

comments