Bondia Manny Pacquiao amemuweka njia panda mkufunzi wake wa muda mrefu, Freddie Roach wakati akijiandaa na pambano lake la Julai 14.

Awali, iliripotiwa kuwa Pacquiao ambaye ameanza mazoezi ya pambano lake na bingwa wa masumbwi ‘welterweight’, Lucas Mtthysse amemfuta kazi Roach na kumpa nafasi aliyekuwa mkufunzi msaidizi.

Jana, Bondia huyo alitoa taarifa rasmi akieleza kuwa bado hajafanya maamuzi ya mwisho kuhusu nani atakayekuwa mkufunzi wake mkuu kwenye pambano hilo.

“Bado sijafanya maamuzi ya mwisho kuhusu nani atakayekuwa mkufunzi wangu mkuu kwa pambano la Julai 14 na Matthysse,” ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

Roach alikuwa mkufunzi wa Pacquiao tangu mwaka 2001 akimtambulisha kwenye ulimwengu wa masumbwi na kung’aa.

Hivi karibuni, Roach alieleza kuwa kila anapompigia Pacquiao simu haipokelewi. “Nilidhani labda amepoteza namba yangu.”

Roach alisema aliumia aliposikia kuwa amefukuzwa kazi na bondia huyo kwani zaidi ya 15 wakiwa pamoja kwenye mapambano yalitengeneza uhusiano wa aina yake.

Pacquiao alisema kuwa kwa muda mrefu mshauri wake Mike Koncz amekuwa akiwasiliana na Roach.

 

Wenyeviti PAC na LAAC wawakosoa Mawaziri kujibu hoja za CAG
Comey amponda Trump, adai hana sifa ya kuwa rais

Comments

comments