Bondia maarufu nchini Ufilipino, Emmanuel Dapidran Pacquiao ‘Manny Pacquiao’ ametangaza  kuwa atawania kiti cha urais kwenye uchaguzi wa mwaka 2022.

Amesema hayo baada ya kuteuliwa na chama chake cha PDP-Laban ambacho ni chama tawala kilicho muweka madarakani Rais wa sasa Rodrigo Duterte.

Uamuzi huo unahitimisha fununu za miezi kadhaa kuwa Pacquiao anagombea wadhifa  wa juu nchini Ufilipino.

Katika hotuba yake ya kukubali uteuzi wa kuwania urais kupitia kundi hasimu ndani ya chama tawala cha Rais Rodrigo Duterte, Pacquiao amesema wakati umewadia wa kushiriki kwenye kinyang´anyiro cha uongozi.

Pacquiao ambaye alijiunga na siasa mwaka 2010 baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge na baadae seneta, ametarajiwa kwa muda mrefu kutangaza nia yake ya kugombea urais nchini Ufilipino.

Rekodi yake kwenye mchezo wa ndondi pamoja na ajenda yake ya kupambana dhidi ya umasikini na rushwa vinatarajiwa muhimu kwenye kampeni yake katika uchaguzi wa mwaka 2022.

Rais wa Zambia asafiri kwa ndege ya abiria
Wapambanaji tukio la Hamza watunukiwa vyeti