Bondia Manny Pacquiao ambaye pia ni Seneta nchini Ufilipino anatarajia kurejea ulingoni Novemba 5 mwaka huu kwa pambano dhidi ya mbabe aliyewahi kupigwa mara moja tu katika mapambano yake 28, Jessie Vargas.

Meneja wa Manny Pacquiao, Koncz amesema kuwa wamejadiliana na Manny Pacquiao na kuamua kumchagua bondia huyo huku akieleza kuwa wamemuacaha Terrence Crawford ambaye watu wengi walikuwa wanampendekeza  kutokana na mtindo anaoutumia.

Jessie Vargas

Jessie Vargas

“Sipendi mtindo anaoutumia Crawford. Siamini kama ni mtindo unaomfaa Manny,” Koncz aliwaambia waandishi wa habari.

Alipoulizwa kama anachohofia ni kasi na namna anavyojilinda bondia huyo, alisema kuwa ni mtindo wake kwa ujumla akiwa jukwaani.

Hivi karibuni, Manny alikanusha tetesi za kurejea jukwaani mwaka huu huku mkufunzi wake pia akidai angependa kama Manny angerudi ulingoni akutane na Floyd Mayweather kwa marudiano, pambano ambalo wengi bado wanalihitaji.

Chelsea Waingia Kwenye Rada Za Arsenal
Video: Shirika la nyumba la taifa latajwa kuchangia uchafuzi wa mazingira