Mlinda mlango chaguo la kwanza kwenye kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba SC Aishi Manula pamoja na Mshambuliaji na nahodha John Bocco huenda wakaukosa mchezo wa mkondo wa kwanza wa mzunguuko wa pili wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika utakaowakutanisha dhidi ya FC Platnum kesho Jumatano, Desemba 23.

Simba itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Taifa mjini Harare nchini Zimbabwe kuanzia majira ya saa 9:00 alasiri kwa saa Afrika Kusini sawa na saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Wachezaji hao walipata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC FC ambao ulishuhudia Simba wakishinda bao 1-0 lilipachikwa kimiani na Meddie Kagere ambaye ametupia jumla ya mabao matano kwa msimu wa 2020/21.

Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa wachezaji hao watafanyiwa tathimini kwenye mazoezi ya leo Jumanne (Desemba 22), ili kujua uwezekano wao wa kuweza kucheza kesho.

Kuhusu wachezaji wengine Barabara amesema wapo vizuri na wanaendelea na maandalizi ya mtanange huo, unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka la Bongo.

Manula alitumia jumla ya dakika 180 kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali dhidi ya Plateau United ya Nigeria ambapo ugenini, Simba ilishinda bao 1-0 na mchezo wa marudio uliochezwa Uwanja wa Mkapa, wawakilishi hao wa Tanzania walilazmishwa sare ya bila kufungana.

Serikali ya Kenya yatishia kuwafukuza kazi wahudumu wa afya
Unabii wa uchumba wazua 'SONGOMBINGO'