Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amemuapisha Mbunge aliyeteuliwa na Rais Magufuli, Prof. Shukrani Manya katika viwanja vya Bunge Chamwino Dodoma.

Mapema leo Rais Magufuli alimteua Profesa Shukrani Manya kuwa Naibu Waziri wa Madini, ambapo Profesa huyo aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Tanzania pia aliteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Manya ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Madini kufuatia aliyeteuliwa awali kushika nafasi hiyo, Mbunge wa Kilwa Kaskazini Francis Kumba Ndulane kushindwa kuapa juzi Desemba 9,2020.

Baada ya kuapishwa kuwa Mbunge, Profesa Manya pia ameapishwa kuwa Naibu Waziri wa Madini, jijini Dodoma.

Ndugai awaita ACT
Mahakama yawaita wadhamini wa Lissu