Mshambuliaji wa Klabu Bingwa nchini Uganda Vipers SC Ceser Manzoki, ameteka vyombo vya habari nchini humo, baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo muhimu za Ligi Kuu.

Manzoki anayemaliza mkataba wake na klabu ya Vipers SC, alikua na msimu mzuri na kufanikiwa kuibeba klabu hiyo hadi kutwaa taji la Uganda 2021/22.

Ijumaa (Juni 17) Mshambuliaji huyo raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, alitangazwa kuwa mshindi wa Tuzo 6 ambazo ni Mchezaji bora wa msimu, Mchezaji bora wa wachezaji, Mshambuliaji bora wa msimu, Mtoa assists bora wa msimu, Kinara wa mabao wa msimu na ametajwa katika kikosi bora cha msimu.

Mafanikio hayo yanatajwa kuendelea kuitamanisha Simba SC ya Tanzania ambayo inatajwa kuwa kwenye mipango ya kumsajili Mshanbuliaji huyo mzaliwa wa DR Congo.

Simba SC inahitaji Mshambuliaji hatari msimu ujao, baada ya safu yake ya Ushambuliaji kuwa butu msimu huu 2021/22 wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao utafikia mwisho mwezi huu.

Tayari Klabu hiyo ya Msimbazi imeshakamilisha dili la kumsajili Mshambuliaji kutoka Zambia Moses Phiri na kumtambulisha kwa Mashabiki na Wanachama wake siku tatu zilizopita.

Mgombea Urais Kenya azomewa nyumbani kwake
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Juni 18, 2022