Waziri wa Nchi, OR- TAMISEMI, Angellah Kairuki amesema Jumla ya maombi 171,916 yakiwemo ya Wanawake 76,190 na Wanaume 95,726 yalipokelewa kwenye mfumo, ambapo maombi ya Kada za Afya yalikuwa ni 48,705 na Kada ya Ualimu ni 123,211.

Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa Waziri huyo, maombi hayo yanafuatia agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutoa kibali cha ajira ya watumishi 21,200 kati yao 13,130 walikuwa wa kada ya Ualimu na 8,070 wa kada za Afya.

Amesema, “mtakumbuka kuwa mwezi Aprili, 2023, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alitoa kibali cha ajira ya watumishi 21,200 kati yao 13,130 walikuwa wa kada ya Ualimu na 8,070 wa kada za Afya.”

Amesema, baada ya kupata kibali cha ajira, Ofisi ya Rais TAMISEMI, ilitoa tangazo kwa wahitimu mbalimbali wa Ualimu na Kada za Afya kuwasilisha maombi ya kazi kupitia mfumo wa kielektroniki wa kupokea na kuchakata maombi ya ajira kuanzia Aprili 12 – 25, 2023.

Aishi Manula aleta mlinda lango mpya Simba SC
Polisi yathibitisha vifo watu watano ajali ya Coaster na Lori