Mahakama Kuu ya Kanda ya Arusha leo inatarajia kusikiliza maombi ya kuongezewa muda wa kuwasilisha notisi ya kukata rufaa kupinga Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kunyimwa dhamana.
Lema amabaye alikamatwa Novemba 2, akiwa Dodoma na kushikiliwa katika Gereza la kuu kisongo Mkoani Arusha kwa siku 36, kutokana na kusudio la Mkurugenzi wa Mashtaka la kupinga kwa Hakimu Mkazi wa Arusha, Desdery Kamugisha aliyempa Lema dhamana katika kesi namba 440 na 441/ 2016 ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Rais Magufuli.
Aidha, Kwa upande wake Wakili Sheck Mfinanga anayemtetea Lema, amesema yeye ndio aliyewasilisha kusudio la kuomba Lema aongezewe muda wa kukata rufaa.
“Ingawa Lema mwenyewe anaomba asikatiwe rufaa,lakini tumeona kwakuwa kuna fursa ya kuwasilisha kusudio hilo la kukayta rufaa,basi tuendelee na michakato ya kisheria”amesema Mfinanga.
Hata hivyo Naibu Msajili, Angelo Rumisha amesema kuwa notisi ya kukata rufaa kwa mshtakiwa alitakiwa awasilishe ndani ya siku kumi tangu uamuzi wa mahakama ulipofanyika.