Maombi ya kufikishwa mahakamani yaliyowasilishwa katika Mahakama Kuu nchini na mawakili wa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu yameanza mchakato kwa kupangiwa Jaji.

Wanasheria wa Lissu wakiongozwa na Fatma Karume waliwasilisha maombi hayo mwishoni mwa wiki iliyopita kwa madai kuwa jeshi la polisi halikumfikisha mahakamani mteja wao baada ya kumshikilia kwa muda mrefu kinyume na sheria.

Taarifa zilizopatikana kutoka katika masijala ya Mahakama Kuu zimeeleza kuwa kesi hiyo iliyofunguliwa chini ya hati ya dharura imepangiwa Jaji Ama-Isario Munisi lakini bado haijapangiwa tarehe ya kusikilizwa.

Lissu alikamatwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Alhamisi ya wiki iliyopita alipokuwa akijiandaa kuelekea jijini Kigali nchini Rwanda kuhudhuria kikao cha wanasheria wa Afrika Mashariki. Polisi wanamshikilia Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kwa tuhuma za uchochezi.

Jeshi la Polisi limesema kuwa litaendelea kumshikilia Lissu hadi pale upelelezi dhidi ya tuhuma zake utakapokamilika ndipo litakapomfikisha Mahakamani.

Jeshi hilo pia lilifanya upekuzi nyumbani kwa Lissu jijini Dodoma ambapo mkewe alieleza kuwa maafisa wa jeshi la polisi waliondoka na CD pamoja na iPad.

Diva The Bawse: Nilidhani kiba angemuoa Jokate.
LIVE: Rais Magufuli aweka jiwe la msingi mradi wa maji kutoka ziwa Viktoria - Tabora