Leo ni siku ya pili ya maombolezo ya kitaifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, baada ya kudaiwa kufanyika mauaji ya halaiki ya raia katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Msemaji wa Serikali ya DRC, anasema idadi ya waliouwawa imeongezeka na kufikia zaidi ya watu 100 ambapo mapema siku ya Alhamis (Desemba mosi 2022), Serikali pia iliwatuhumu waasi wa M23 kuwauwa watu 50 katika kijiji cha Kishishe kilichopo kilomita 70 kaskazini mwa mji wa Goma.

Maisha katika ukanda wa mashariki mwa mji wa Goma nchini DRC. Picha ya UN.

Hata hivyo, kundi hilo la waasi lilikanusha madai hayo kwa kusema hayana msingi na kusema kamwe hawawezi kuwauwa raia na kudai kuwa hawapo tayari kuangamiza upande usio na hatia.

Desemba 2, 2022 katika mkutano wa baraza la mawaziri, Rais Felix Tschisekedi alilaani kwa maneno makali mauaji hayo ya Kishishe, na kutoa amri ya kufanyika maombolezo ya kitaifa ya siku tatu sambamba na bendera kupepea nusu mlingoti.

Waliokuwa mateka wakutanishwa na familia zao
TAWA yatekeleza agizo la Rais udhibiti wanyama wakali, waharibifu