Maoni ni sehemu muhimu ya ukuaji na utendaji wa kazi zako kitaaluma. Yanasaidia kukuonyesha ikiwa utendaji wako ni mzuri au mbaya na ni maeneo gani unapaswa kuboresha. Kupokea maoni hasi kazini inaweza kuwa ni kitu kigumu kusikia, lakini ni fursa ya kujifunza na kutumia somo utakalolipata kuwa mfanyakazi mzuri zaidi.

Kuweza kugeuza maoni hasi kuwa kitu chanya ni hatua muhimu kwa mafanikio ya kazi zako. Hizi ni njia 6 za kukabiliana na maoni mabaya juu ya kazi yako:

  1. Chukua Muda Wa Kutosha Kutafakari

Ule wakati wa kukosolewa na kupewa maoni juu ya kazi yako, unaweza kuwa na hisia sana. Unaweza kukasirika na kuhuzunika. Inawezekana pia ukashindwa kuendelea kumsikiliza bosi wako au ukachagua kujibishana nae. Hii inaweza kukufanya ukose maelezo ya muhimu au kusababisha kutokuelewana. Ni muhimu kujipa wakati na nafasi ya kutosha ili kuchuja na kupokea vyema maoni hayo. Hii itakusaidia kupata muda mzuri kufikiria juu ya hali hiyo kwa uwazi zaidi na kupanga majibu yanayojiridhisha. Unaweza kuomba muda wa kukusanya mawazo yako kabla ya kujibu maoni hayo.

 

2. Chuja na Uchukue Vitu Chanya Tu

Maoni ni kitu muhimu kwa ukuaji wako binafsi na wa kitaaluma. Hata wakiyawasilisha kwa njia nzuri au mbaya, meneja au mfanyakazi mwenzako watakupa maoni mabaya ili uweze kufanya kazi bora zaidi. Ili kusimama imara juu ya taaluma yako, chagua kutenga na kuchukua maoni chanya na ufanyie kazi bora zaidi.

  1. Fikiria Kuwa Wanakukosoa Kwa Nia Nzuri

Njia nyingine ya kubakia kuwa mchapakazi hata baada ya maoni hasi ni kwa kufikiria juu ya nia njema ya bosi au mfanyakazi mwenzako kwanza. Maoni ni ishara kwamba wanataka kukusaidia kufanya kazi bora ambayo itasababisha kufanikiwa katika kazi yako. Ikiwa utaona kuwa watoa maoni wana nia nzuri na wanaweza kukusaidia kuleta matokeo bora, itakuwa rahisi kwako kufanya mabadiliko mazuri.

  1. Kuwa Mtulivu na Sikiliza kwa Makini

Kubishana na mfanyakazi au meneja wako kwa sababu ya maoni yao, hata kama ni hasi haitasaidia. Wanaweza kuwa na mawazo ambayo yangekusaidia kufanya kazi bora, lakini wakashindwa kufanya hivyo. Badala ya kujitetea sana au kupambana na kubishia maoni yao, jaribu kuwasisitiza kwa upole wakupe maelezo zaidi. Uliza maswali kama ‘Unaweza Kunipa ufafanuzi zaidi? Una sampuli ya kazi kama hiyo? Unaweza kunionyesha mfano ili nifanye vizuri zaidi?’ Kwa njia hii, utakuwa na uwezo wa kuifanya kazi hiyo vizuri zaidi.

  1. Kuwa Makini na Jifunze

Inapotokea unapata matokeo mabaya ya kazi yako pamoja na maoni hasi, unapaswa kuepuka kuanza kuelezea jinsi wengine wamehusika. Itakupotezea muda na kukupunguzia kasi ya kujifunza kutoka makosa na uwezekano wa kurekebisha kosa. Zingatia mpango wako unaofata na tumia fursa hii kufikiria njia ambazo utatumia kurekebisha kazi, tabia na mtazamo wako.

  1. Wanakosoa Kazi Yako, Sio Wewe

Kugundua makosa kwenye kazi yako mwenyewe inaweza kuwa kazi ngumu. Unapomaliza, huenda usijue wapi pa kurekebisha na wapi pa kuacha. Hivyo, wakati meneja au  mfanyakazi mwenzako anaelezea makosa hayo, badala ya kuchukia, unapaswa kumshukuru badala yake. Daima kumbuka kwamba hawa wanakosoa kazi yako na si wewe. Kukubali kwa moyo na akili moja maoni hayo, na uulize kama wana wazo bora juu ya namna unaweza kuboresha kazi yako.

Kukosolewa na maoni hasi ni fursa nzuri ya kumwonyesha mwajiri wako kwamba unaweza kubadilika na kufanya mabadiliko muhimu. Unapokosolewa, chukulia kama ni nafasi ya kuboresha utendaji wako na utayari wako wa kurekebisha makosa yoyote.

Serikali yanunua mashine mpya ya kutoa tiba ya mionzi
Wanusurika kifo baada ya Ndege kudondoka baharini