Mchungaji wa kanisa la Emmaus Bible Church lililopo Mbezi jijini Dar, Daudi Mashimo siku chache zilizopita alithibitisha kushikiliwa na polisi kituo cha Oysterbay kwa masaa kadhaa kutokana na maono yake kuhusu kifo cha mtangazaji wa kipindi cha Jahazi wa Clouds FM, Ephraim Kibonde kilichotokea Machi 7 mwaka huu.

Ambapo kwa mujibu wa mchungaji huyo alidai kuwa Mungu wake alimuonesha kuwa Ephraim Kibonde hakufariki dunia kama ambavyo inafahamika na kusema kuwa walizika mgomba.

“Unajua watu wanashindwa tu kunielewa kwamba si mimi bali ni Mungu mwenyewe anasema kupitia mimi. Nime­shaoneshwa mambo mengi huko nyuma nikayasema na kweli yakadhihirika mbona watu walikuwa hawashangai” amesema Mchungaji Mashimo.

Kufuatia uvumi huo jeshi la polisi liliamua kumuita na kufanya nae mahojiano kwa masaa kasaa juu ya kauli na maono yake kuhusu kifo cha Kibonde kwani endapo maono yake yangeendelea kuvuma ingeweza kuleta madhara makubwa kwa jamii na hasa familia.

Hivyo polisi walimshikilia na kumstopisha kusambaza habari hizo ambazo zingeweza kuchonganisha, mara baada ya Mashimo kuachiliwa na polisi aliendelea kuwa na msimamo wake na kusema kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu tu hawezi kuacha kutoa unabii.

“Kwa hili la kifo nasima­mia msimamo wangu, yaani mpaka kesho huo ndio unabii wangu, mimi ni mtumishi wa Mungu nini kosa langu…ni maono hata kama wameni­piga marufuku siwezi kuacha kutoa unabii, nitaendelea kumsikiliza Mungu tu, haya ndio maisha yangu hivyo siwezi kuacha kuongea kile ambacho Mungu amenione­sha,” alisema mchungaji.

Naye Kamanda wa Kinondoni, Mussa Athumani Taibu amethibitisha wito huo na kiusema;

“Tulimwita kwa shida zetu akidaiwa kusema kuwa Kibonde hajafa, wamezika mgomba anaweza kuleta uchonganishi kwa familia ikapelekea ramli chonganishi ambayo huleta maafa, hatu­jamzuia kufanya mikutano wala kuhubiri neno au ma­fundisho ya Mungu. Hicho tu ndicho tulichomwitia,” alisema kamanda Musa.

 

 

'Happy Birthday' Mkuu wa Wilaya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwagelo
Simba yaendeleza ubabe, yairarua Ruvu Shooting 2 - 0