Tanzania kwa kushirikiana na Ufaransa inatarajia kuonesha mapishi tofauti ya asili za nchi mbali mbali mnamo Machi 21, mwaka huu.

Ubalozi wa Ufaransa nchini kwa kushirikiana na wadau wa Hoteli ya Hyatt Regacy ndio waandaaji wa maonesho hayo na wanatarajia kufanya hafla ya kihistoria ya sanaa ya upishi wa vyakula.

Lengo kuu la hafla hiyo ni kupeana ushirikiano na uzoefu kutoka kwa wapishi wa hapa nchini na wamataifa mbali mbali duniani kuweza kujua namna bora ya kuandaa vyakula bora vyenye kuwavutia walaji.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa mawasiliano  na masoko wa hoteli hiyo Lilian Kisasa, amesema kuwa hafla hiyo itahudhuliwa na wapishi zaidi ya 5,000 wakiwepo kutoka  Ufaransa.

Kwa upande wa Tanzania itawakilishwa na mpishi mmoja kutoka hoteli hiyo Francious Lucchesi ambaye ataonesha jinsi mapishi ya tanzania yalivyo na vyakula vya asili.

Tukio hilo ni mara ya kwanza kufanyika hapa nchini lakini tayari limesha fanyika maratano katika nchi nyingine na katika hafla hiyo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Balozi wa Ufaransa nchini, Fredric clavier pamoja na wadau mbali mbali nchini ili kushuhudia utaalamu wa uandaaji wa mapishi.

Naye Mkurugenzi mkuu wa hoteli hiyo, Garry Fried amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kwani hakuna kiingilio na watajifunza tamaduni mbali mbali za mapishi, pia linalenga kutengeneza ajira na kutoa ushawishi kwa watalii kuja nchini.

 

Naibu Waziri Mabula awageuzia kibano wakuu Idara ya Ardhi
Kula vyakula hivi kuokoa Nywele zako