Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt. Batilda Burian amesema suala la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga si jukumu la Wizara ya Afya pekee na kwamba ni muhimu kila sekta kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na tatizo hilo.

Batilda ameyasema hayo katika ufunguzi wa kikao cha watalaam wa Afya Kanda ya Magharibi, inayounda mikoa ya Tabora, Katavi na Kigoma cha kujadili mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga katika kanda hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Batilda Burian akizungumza na wataalam wa Afya kanda ya Magharibi katika ufunguzi wa kikao hicho cha 
kujadili mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kwa mikoa ya Tabora,Katavi,na Kigoma.

Amesema, “maelekezo ya Wizara ya Afya ni kuhakikisha kila Halmashauri inaweka mikakati ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga, hivyo suala hili si la Wizara ya Afya ni la sekta zote tusimamie masuala ya Afya ya msingi na afya ya uzazi na watoto ili vifo hivi vipungue.”

Dkt. Batilda ameongeza kuwa, sababu zinazochangia vifo ni kutokana na kupoteza damu nyingi kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua ,sasa tunafanyaje watu wa kilimo wanafanyaje,katika bustani zao wanakuwa na mbogamboga ,rozela inayosaidia kuongeza damu.

Clatous Chama abaki Dar es salaam
Anayedhibiti mbegu anaweza kukutawala: Bashe