Uongozi wa klabu ya Simba umepingana na mapendekezo yaliyowasilishwa kwao na kocha mkuu wa klabu hiyo Jackson Mayanja siku ya jumatano, ya kukiboresha kikosi cha wekundu hao huku akitaka idadi kubwa ya wachezaji waondolewe.

Mmoja wa mabosi wa juu Mtaa wa Msimbazi (jina linahifadhiwa), alikaririwa akisema kuwa, mapendekezo mengine ya Mayanja ni kuitaka klabu hiyo kutosajili wachezaji wa kigeni kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki.

Mayanja amewaponda wachezaji kutoka ukanda huo akidai kuwa ni wasumbufu na hawana viwango vya kutisha.

“Bado tunaendelea na kikao muda huu, lakini kwa ufupi mapendekezo ya Mayanja hayatekelezeki,” alisema bosi huyo.

Ili kutimua idadi kubwa ya wachezaji kama ilivyopendekezwa na Mayanja, Simba itahitaji kiasi kikubwa cha fedha kulipa fidia ya kuvunjwa mikataba, lakini pia itahitaji fedha nyingi kufanya usajili, jambo ambalo uongozi umeona haliwezekani.

Nyota anaotaka Mayanja wabaki ni pamoja Vicent Angban, Peter Manyika, Justice Majabvi, Said Ndemla, Novatus Lufungo, Jonas Mkude, Awadh Juma, Danny Lyanga, Hassan Isihaka na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

Copa America 2016 - Kaka Kuziba Pengo La Douglas Costa
Gabriel Omar Batistuta Amkingia Kifua Francesco Totti

Comments

comments