Kapteni Ibrahim Traore, ametangaza kupitia televisheni ya taifa la BurkinaFaso kuwa ameupindua utawala wa Rais Paul-Henri Damiba ambaye naye ni kiongozi wa Kijeshi aliyeingia kwa kumpindua Rais Marc Kaboré, Januari 24 mwaka huu.

Wanajeshi hao, chini ya Kapteni Ibrahim Traore, pia wamevunja Serikali, kusimamisha na kuweka katiba ya mpito na Kapteni Ibrahim Traore amesema wamemuondoa Damiba baada ya kushindwa kukabiliana na uasi unaozidi kuota mizizi kinyume na ahadi zake za kuifanya Nchi kuwa salama zaidi.

Hili, linakuwa ni tukio la pili la Mapinduzi ya Kijeshi ndani ya Miezi 8, ambapo Damiba alifanya mapinduzi Januari 2022 yaliyomuondoa Madarakani, Roch Marc Kaboré, Rais aliyechaguliwa Kidemokrasia, huku Serikali ikisema tukio hilo linahusishwa na mgogoro wa ndani katika jeshi hilo.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali Lionel Bilgo mgogoro uliopo umetokana na madai yanayohusishwa na mishahara na kwamba mtawala wa kijeshi Luteni Kanali Paul Sandaogo Damiba anashiriki kwenye mazungumzo ya kutafuta muafaka na wanaohusika.

Awali, mkuu wa chama tawala Junta nchini Burkina Faso Luteni Kanali Paul-Henri Damiba akitoa wito hapo jana juu ya Utulivu tangu ripoti za awali za milio ya risasi na uwepo mkubwa wa kijeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi. 

Kanali Damiba, aliongeza kuwa mazungumzo yanafanyika ili kurejesha utulivu, akisema kuwa “adui anayeishambulia nchi anataka kuzusha mifarakano kati ya watu wa Burkina Faso ili kuivuruga nchi.” lakini inaonekana kauli hii imeshindwa kuzaa matunda baada ya nchi kupinduliwa tena usiku wa Octoba Mosi.

Bilioni 30 kulipa fidia wananchi Kabanga Nickel
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Octobar 1, 2022