Mkoa wa Dodoma umeahirisha maandalizi ya mapokezi ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyekuwa akitarajiwa kuhamia rasmi leo mjini humo.

Mkuu wa Mkoa huo unaotarajiwa kuwa makao makuu ya Serikali, Jordan Rugimbana amesema kuwa wameahirisha tukio hilo na kwamba litafanyika baada ya kumalizika kwa vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litakaloanza mapema wiki ijayo.

Waziri Mkuu, Majaliwa alitangaza kuwa atahamia Dodoma mwezi huu ikiwa ni sehemu ya kuongoza utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuihamishia Serikali yote mjini humo ndani ya kipindi cha utawala wake.

Serikali ya Mkoa huo iliitangaza Septemba 1 kama siku ya kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu mkoani humo. Mapokezi hayo yalipangwa kuwa na maandamano katika baadhi ya mitaa ya mji huo hadi  katika eneo la uwanja ambapo angewahutubia wenyeji wake.

UVCCM yaivaa rasmi Chadema kwa kushindwa kufanya UKUTA
Mbwana Samatta: Nitawasiliana Na Daktari Wa Taifa Stars