Mamlaka za Tibet zimearifu kupatikana kwa miili zaidi na kufanya idadi ya waliofariki kwa maporomoko ya milima ya theluji iliyoyafukia magari kwenye eneo la barabara kuu kufikia watu 28.

Shughuli za kuondoa theluji katika eneo la kutokea barabara kuu ya chini kwa chini inayounganisha mjini wa Nyungchi iliyopo kusini magharibi mwa Tibet na eneo yalikotokea maporomoko bado zinaendelea ili kuweza kuopoa miili zaidi.

Shughuli za uokoaji zikiwa zinaendelea huko Tibet.

Jumla ya waokoaji zaidi ya 1,000 wamejiunga ili kuongeza nguvu na usaidizi wa kutafuta watu waliofukiwa na maporomoko hayo yaliyoleta madhara, ambapo wengi wa waliofariki na walikuwa wakirudi katika miji yao kwa ajili ya sherehe za Mwaka Mpya za Lunar, ambayo inaanza hapo kesho Jumapili Januari 24, 2023..

Hadi kufikia jana Ijumaa (Januari, 20 2023), watu 20 walikuwa wamethibitishwa kufariki na wanane ambao miili yao imepatikana walikuwa hawajulikani walipo, huku watu 53 wakiokolewa watano kati ya walionusurika wakijeruhiwa vibaya.

CCM yaibana Wizara vishikwambi vya Walimu
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 21, 2023