Marekani ni Taifa lenye nguvu za kiuchumi, kijeshi na ushawishi mkubwa Duniani huku likiwa pia ni Taifa ambalo halipendwi kutokana na baadhi ya maamuzi yake ambayo wwakati mwingine hutafsiriwa kama yanaingilia utamaduni, kuvuruga mipango na maamuzi ya Mataifa mengine.

Uhusiano mzuri wa taifa moja na jingine kidiplomasia husaidia kuepusha mifarakano na kurahisisha shuguhuli na utendaji wa kimataifa baina ya nchi moja na nyingine, lakini kwa Marekani hali ni tofauti kwani pamoja na sifa ilizonazo, bado Taifa hilo limekuwa likipitia misukosuko mingi ya alama za kudumu.

Jambo la kwanza ambalo Marekani haitasahau, ni lile la mwaka 1970 la kuibuka kwa vuguvugu la kiutawala baada ya vijana wa nchi hiyo kuupinga utawala wa Mohammed Reza Shah Pahlavi na kusababisha maandamano na ghasia kuonyesha kuchoshwa na utawala wa kiongozi huyo wa kukaa madarakani kwa muda mrefu.

Shambulio la ndege zilizotekwa zilizopiga majengo mawili ya kibiashara nchini humo. Picha na JOSE JIMENEZ/GETTY IMAGE.

Julai 1979 Reza Shah Pahlavi, alilazimika kuachia ngazi na kukimbilia nchini Misri na ndipo Ayatollah Ruhollah Khomeini akaingia madarakani, kitendo ambacho kikasababisha kundi la wanafunzi wa Iran Novemba 4, 1979, kuvamia ubalozi wa Marekani ulioko Tehran, na kuteka zaidi ya Wamarekani 60.

Jambo la pili, ni kushambuliwa kwa ubalozi wa Marekani nchini Libya, hili likawa pigo jingine, kwani Septemba 11 na 12 mwaka 2012, katika ubalozi wake mjini Benghazi, wapiganaji wa Kiislam walivamia, kushambulia na kusababisha vifo vya Wamarekani wanne akiwemo Balozi wake wa nchini Libya, John Christopher.

Wapiganaji hao, walikuwa sehemu ya Walibya waliokuwa wanataka mabadiliko lakini pia kupinga kuingiliwa kwa nchi hiyo na mataifa ya nje ikiwemo Marekani, na kifo cha Balozi Christopher kikawa cha kwanza kilichotokana na kushambuliwa tangu mwaka 1988.

Uokoaji wakati wa shambulio la Ubalozi wake wa Benghazi nchini Libya. Picha na Reuters.

Balozi Christopher aliteuliwa mei 2012 kuongoza ofisi za ubalozi mjini Tripoli lakini alienda Benghazi kwenye makazi madogo ya balozi wa wamarekani kwa ajili ya shughuli maalumu, na usiku wa septemba 11, wanamgambo wa kiislam zaidi ya 150 wanaohusihwa na kundi la Al-qaeda walivamia na kushambulia.

Jambo la tatu ni kifo cha John Kennedy, rais wa 35 wa taifa hilo kuanzia mwaka 1961 mpaka 1963 akiwa mzaliwa wa familia ya kitajiri toka Brooklyn, Massachusetts na wakati wa utawala wake alikuwa na ushawishi mkubwa na kinara wa vita baridi akielekeza nguvu zake kwenye mahusiano ya Muungano wa Soviet na Cuba.

Kifo chake kiliacha simanzi kubwa kwa Wamarekani, alikuwa na dhamira ya kuleta mabadiliko akipanga kuuondoa utawala wa Rais Fidel Castro wa Cuba ulioonekana kuwa tishio kwa usalama wa Marekani, na aliuawa kwa kupigwa risasi Dallas, Texas Novemba 22, 1963 na mwanajeshi wa zamani wa majini, Lee Harvey Oswald ambaye alitiwa nguvuni na kuuawa na mtu anayeitwa Jack Ruby, siku mbili baadae.

Mwanajeshi wa zamani, Lee Harvey Oswald akadaiwa kutekeleza mauaji ya Rais wa 35 wa nchi hiyo. Picha na GETTY IMAGES.

Kuibuka kwa janga anga la Uviko-19 mwishoni mwa mwaka 2019, kukaleta taswira ya nne isiyosahaulika kwa Taifa hilo, japo kwa kiasi kikubwa liliathiri mataifa mengi ulimwenguni, lakini yenyewe ilikuwa na athari zaidi kutokana na idadi kubwa ya visa vilivyokifikia milioni 40.5 na vifo zaidi ya 662,000.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za vyombo vya Habari, kinachoisumbua Marekani kutokana na Uviko-19 ni upungufu wa ajira, kutokana na zaidi ya watu milioni 20.5 kupoteza ajira katika kipindi cha chini ya miaka miwili ya uwepo kwa janga hilo na tangu December 2019, uzalishaji wa bidhaa na biashara haujakaa sawa.

Hatua hii, inatokana na Taifa hilo kuwekeza nguvu zake nyingi kutoa chanjo ya corona kwa watu wake na kusaidia nchi na kuzisaidia nchi zinazoendelea, ili kuendelea kujiweka sawa na kuwa salama tayari kwa kurejesha heshima na nafasi yake kiuchumi Duniani.

Shambulio hili la ndege zilizotekwa lililoacha zaidi ya majeruhi 10,000 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 3,000. Picha na GETTY IMAGES.

Leo ni miaka 21, toka tukio la Septemba 11, 2001 la ‘Mkono Shavuni’ kwa Taifa la Marekani kupata shambulio la kigaidi lililosababisha vifo vya watu zaidi ya 3,000 baada ya Washambuliaji wa kujitoa muhanga kuteka ndege nne za shirika la ndege la nchini humo.

Ndege hizo, zilitumiwa na watekaji kushambulia kwa kuzibamiza kwenye majengo makubwa mawili yaliyokuwa sehemu ya uso wa Taifa la Marekani ambayo ni Jengo la Biashara la New York trade Center na Makao Makuu ya jeshi la Marekani, Pentagone.

Zaidi ya majeruhi 10,000 walipatikana katika shambulio hilo ambalo liliisumbua Marekani kwa muda mrefu na kuamua kuendesha shughuli zake kijeshi katika nchi za Iraq na Afghanistan hadi ilipofanikiwa kumuuua Kiongozi wa Al qaeda, Osama Bin Laden na kuuondoa utawala wa Saddam Hussein nchini Iraq.

Janga la Uviko-19 likaibua majonzi mengine kwa Taifa hilo na Dunia kiujumla.

Hata hivyo, ukiachilia mbali mzozo kati ya Marekani na Urusi, yapo mataifa mengine yenye uhasana wa ‘Chui na Paka’, ambayo kwa muda mrefu uhusiano wao wa Kidiplomasia ni mbovu ikiwemo Israel & Palestina, China & Japan, Iran & Saudi Arabia, Korea ya Kaskazini & Korea ya Kusini, India & Pakistan, Uingereza & Ufaransa, Uingereza & Ireland, Ujerumani & Ufaransa na Uturuki & Ugiriki.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 12, 2022 
Wazazi watakiwa kufanikisha Mabaraza ya Watoto