Wahamiaji Haramu 36 Raia wa Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na DRC Congo wanashikiliwa na Idara ya Uhamiaji mkoa wa Mara kwa makosa mbalimbali.

Makosa hayo ni pamoja na kughushi vyeti vya kuzaliwa na kufanikiwa kupata ajira katika Taasisi za Umma ikiwemo sekta ya Afya, TRA na Elimu Kinyume cha sheria za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Naibu Kamishina wa Uhamiaji Mkoa wa Mara Albert Rwelamira amesema kuwa baadhi ya watuhumiwa wamekutwa na Vitambulisho vya taifa na wengine vya ujasiriamali vilivyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Serikali yapokea msaada wa Bilionea Jack Ma, vifaa vya kukinga Corona
Uhispania: Maiti za wazee waliokufa kwa Corona zakutwa kwenye makazi

Comments

comments