Gwiji wa soka duniani Diego Armando Maradona, amewashauri mastaa wa soka kwa kusema huu ndio wakati sahihi kutoa sehemu ya utajiri wao kusaidia kupambana na virusi vya Corona.

Maradona raia wa Argentina akaenda mbali zaidi kwa kusema kuna baadhi ya wachezaji hawastahili hata kulipwa mshahara wakati huu wa janga la Corona lakini pia amevikosoa baadhi ya vilabu vinavyo wachukulia wachezaji wao kama watumwa.

“Kuna baadhi ya wachezaji ambao hata hawastahili kulipwa (wakati huu wa Corona), hiyo ni kweli na wote tunajua hilo lakini kuna wachezaji pia ambao hawawezi kucheza bure hata kwa mwezi mmoja vilabu vinapaswa kuwalipa” – Maradona

”Lakini kuna baadhi ya klabu ambazo kwa sasa zinafanya ujinga zinataka kutumia haya majanga (Corona) kama njia ya kutowalipa wachezaji wake, wanawachukulia wachezaji kama watumwa kwa miaka, inaonekana kama kuna baadhi ya vilabu siku zote kama kuna gonjwa la mlipuko vile” alisema Maradona

Mfumo mpya Young Africans kukamilika mwezi ujao
Waziri wa Afya ashushwa cheo kwa kuipeleka familia baharini