Wakati wananchi nchini Madagascar wanafanya uamuzi kuhusu nani awe Rais wao, takribani wagombea 36 wamejitokeza kuwania kiti hicho huku wanne wakiwa ni ma rais wa zamani wa nchi hiyo ambao wanataka kurejea tena madarakani kuongoza kisiwa hicho.

Wagombea wengine waliojitokeza ni mawaziri wakuu wawili waliowahi kuiongoza nchi hiyo, Wachungaji na mwimbaji wa muziki wa pop kisiwani humo.

Kwa upande wa Rais wa sasa, Hery Rajaonarimampianina naye ana tetea kiti chake cha Urais, na atakabiliana pia na watangulizi wake wawili Marc Ravalomanana ambaye ni tajiri wa biashara ya maziwa na alitawala mwaka 2002 hadi 2009, huku Andry Rajoelina aliye fahamika kama DJ ambaye alitawala hadi 2013.

Aidha, Madagascar ilikumbwa na mgogoro wa kisiasa baada ya uchaguzi wa mwaka 2001 ambapo matokeo yalisababisha mapigano, huku mwaka 2009 yakitokea mapinduzi yaliyoungwa mkono na jeshi ambapo yalimuondoa madarakani Ravalomanana.

Hata hivyo, mbali ya maandamano yaliyofanyika mapema mwaka huu, kwa kiasi kikubwa utawala wa Rajaonarimampianina umekuwa wa amani, lakini hasira juu ya mambo yaliyopita bado inaonekana.

 

Al Ahly kupinga adhabu ya Walid Azaro
Romelo Lukaku kuikosa Juventus FC