Marais Wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamehudhuria Mkutano Mkuu wa 39 unaofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kushuhudia Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, Dkt. John Magufuli akikabidhiwa Uenyekiti wa jumuiya hiyo.
 
Marais hao Wastaafu ambao wamehudhuria ni Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye ni Rais wa Serikali ya Awamu ya Pili, Benjamin Mkapa ambaye ni Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Jakaya Kikwete aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne na kwa upande wa Zanziabar Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Amani Karume.
 
Mbali ya wastaafu hao kuwepo kwenye mkutano huo ambao pia wametambulishwa kwa wageni mbalimbali kutoka nchi 15 za jumuiya hiyo, pia viongozi wengine wa Serikali ya Tanzania waliohudhuria ni Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
 
Wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Balozi John Kijazi, Mawaziri, viongozi wa ngazi mbalimbali wastaafu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
 
Nafasi hiyo ya Uenyekiti wa SADC kwa Tanzania mara ya mwisho ilishikiliwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa miaka 16 iliyopita na sasa amekabidhiwa Rais Dkt. Magufuli.
Hata hivyo nchi mbalimbali za jumuiya hiyo zimeonyesha matumaini na imani kubwa kwa Rais Magufuli hasa kutokana na utendaji wake tangu akiwa Rais ambaye anaamini katika wananchi kufanya kazi na nchi kujitegemea.

Rais Magufuli kuanza na vikwazo vya Zimbabwe
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake SADC asisitiza ajira kwa vijana