Nahodha na beki wa Man City, Vincent Jean Mpoy Kompany, ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ubelgiji, ambacho hii leo kitapambana na timu ya taifa ya Italia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Kompany, ameshindwa kupita katika vipimo vya afya alivyofanyiwa jana jioni, baada ya kuumia kiazi cha mguu akiwa katika mazoezi ya mwisho ya timu ya taifa lake ambalo kwa sasa linashika nafasi ya kwanza kwenye viwango vya ubora wa soka duniani.

Kompany, pia ataukosa mchezo mwingine wa kimataifa wa kirafiki ambao utachezwa kati kati ya juma lijalo ambapo Ubelgiji watachuana na timu ya taifa ya Hispania.

Hata hivyo kuna uwezekano kwa beki huyo akarejea uwanjani mwishoni mwa juma lijalo, katika mchezo wa ligi ya nchini Engalnd, ambapo Man City watakuwa wenyeji wa Liverpool kwenye uwanja wa Etihad.

Meneja wa Man City, Manuel Pellegrini ameonyesha kuzipokea kwa mshtuko taarifa za kuumia kwa nahodha wa kikosi chake, kwa kudai kwamba, Kompany amekua na bahati mbaya ya kuumia mara kwa mara.

Kompany, alikosa michezo miwili iliyoihusu klabu ya Man City mmwezi uliopita dhidi ya Bournemouth pamoja na Sevilla, lakini alipata nafasi ya kurejea kikosini wakati wa mchezo dhidi ya Manchester United uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford.

Jamie Vardy Kumkalisha Benchi Wayne Rooney
Raia Wa Liberia Aondolewa Kwenye Kinyang'anyiro