Kocha aliyeipa mafanikio timu ya taifa ya Italia katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2006, kwa kuiwezesha kutwaa ubingwa wa dunia,  Marcello Lippi amesema kwamba anavyoona Carlo Ancelotti ndiye bora katika ulimwengu wa sasa kuliko wenzake wenye majina, Pep Guardiola na Jose Mourinho.

Ancelotti (pichani juu) ndiye atakayemrithi Guardiola, Bayern Munich ifikapo mwishoni mwa msimu huu, baada ya kuamua kutoendelea kuwafundisha mabingwa hao wa Ligi ya Bundesliga.

Lippi ana imani kubwa na kocha huyo ambaye amewahi kuzinoa timu kubwa na kuzipa ubingwa kama vile AC Milan, Chelsea, Paris Saint-Germain na Real Madrid.

“Ancelotti ni kocha bora katika ulimwengu wa sasa,” Lippi aliuambia mtandao wa II Messaggero.

“Amewahi kutwaa mataji mengi akiwa mchezaji na akiwa kama kocha Italia na nje ya Italia,” alisema Lippi.

Uwanja Wa Amani Zanzibar Waandika Histoaria Mpya
Mwinyi Haji Ngwali Afurahishwa Na Mapinduzi Cup