Beki wa kushoto kutoka nchini Brazil na klabu ya Real Madrid Marcelo Vieira da Silva Júnior, amekanusha uvumi wa kuwa mbioni kuondoka mjini Madrid, kwa kusema hafikirii kufanya hivyo, zaidi ya kuamini atamaliza soka lake akiwa na mabingwa hao wa barani Ulaya mara tatu mfululizo.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 30, amekua akihusishwa na taarifa za kutaka kumfuata Cristiano Ronaldo aliehamia klabu ya Juventus FC ya Italia miezi mitatu iliyopita.

“Ninafuraha ya kucheza soka langu hapa (Madrid),” alisema Marcelo alipohojiwa na mwandishi wa habari wa tovuti ya AS.

“Watu wanafahamu nini ninachokipata katika soka langu nikiwa hapa, bado nina muda mrefu wa kuendeea kuwepo hapa, kutokana na mkataba wangu unavyojieleza, kwa ufupi ninafurahia sana maisha ya mji huu na klabu yangu.”

“Sidhani kama kuna klabu kubwa na bora kama Real Madrid, Siku zote ninapenda kuwa miongoni mwa wachezaji wanaoitumikia klabu kubwa duniani.

“Japo inapendeza kuhusishwa na klabu nyingine, kwa sababu ninaamini mpaka suala hili linaibuliwa, huenda upande wa pili wanakujadili katika vikao vyao na kukuona unawafaa katika mipango ya kikosi chao, lakini msisitizo wangu nitaendelea kuitumikia Real Madrid, na ikiwezekana nitamalizia soka langu nikiwa hapa.”

Marcelo alisajiliwa na Real Madrid Januari 2007 akitokea klabu ya Fluminense ya nchini kwao Brazil, na tayari ameshawatumikia mabingwa hao wa Ulaya mara tatu mfululizo katika michezo 456.

Akiwa na klabu hiyo amefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ulaya mara nne, mataji manne ya ligi ya Hispania (La Liga) na kombe la Mfalme (Copa del Reys) mara mbili.

PPRA yawapa wahandisi ufafanuzi fursa ya ununuzi kwa njia ya mtandao
Video: Ni lazima King'anya akamatwe- JPM