Aliyekua meneja wa klabu ya Olympique de Marseille inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa, Marcelo Bielsa anatajwa huenda akawa mkuu wa benchi la ufundi la Swansea City kuanzia msimu ujao.

Gazeti la The Mirror la nchini England, limeeleza kwamba Bielsa anatajwa kurejea katika tasnia ya ufundishaji soka kuanzia msimu ujao, baada ya kuwa pembeni kwa zaidi ya muda wa miezi minane.

Fununu za kuajiriwa kwa meneja huyo kutoka nchini Argentina, zimeibuka kufutia muwekezi mpya ambaye anatarajiwa kuinunua Swansea city kwa kiasi cha Pauni million 140 mwishoni mwa msimu huu.

 Brendan Rodgrers

Hata hivyo Bielsa, huenda akapata wakati mgumu katika mchakato wa kupata ajira huko Liberty Stadium, kutokana na bosi wa sasa wa klabu ya Swansea City Francesco Guidolin kumpendekeza Brendan Rodgers, ili aweze kurejea katika majukumu yake.

Rodgers alifanikisha safari ya Swansea City kucheza ligi kuu msimu wa 2011-12 baada ya kufanya vyema katika ligi daraja la kwanza.

Kwa sasa kikosi cha Swansea City kinanolewa na meneja kutoka nchini Italia Francesco Guidolin ambaye amepewa jukumu hilo hadi mwishoni mw amsimu huu.

Real Madrid Kuziingiza Vitani Chelsea Na Manchester United
Anne Kilango asema haya baada ya Rais Magufuli kumtimua ‘Ukuu wa Mkoa’