Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil Tite, amesema beki wa pembeni Danilo amerejea katika mazoezi ya kikosi chake, huku kukiwa na matumaini hafifu ya kumtumia beki wa kushoto na nahodha Marcelo katika mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Mexico.

Marcelo, bado hajashiriki mazoezi na wachezaji wenzake tangu alipoumia bega wakati wa mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Serbia, jambo ambalo linaendelea kuumiza vichwa vya madaktari wa kikosi cha Brazil.

“Marcelo bado hajawa tayari kufanya mazoezi na wenzake, jopo la madaktari linaendelea kufanya kazi yake ili kufanikisha lengo la kumuweka sawa na kurejea katika hali yake ya kawaida.

“Ninaamini kabla ya mpambano wetu na Mexico atakua sawa na huenda nikamtumia katika mipango yangu, ili tufanikishe lengo la kupata matokeo mazuri.” Amesema Tite

Kwa upande wa Danilo aliyekua anasumbuliwa na jeraha ya paja, jana ijumaa amerejea katika mazoezi na wenzake na ameonyesha kuwa FIT kuelekea mchezo dhidi ya Mexico ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa.

Brazil wataikabili Mexico katika mchezo wa hatua ya 16 bora, utakaochezwa Julai mbili kwenye uwanja wa Cosmos, uliopo mjini Samara

Video: Dogo Janja aachia ngoma mpya 'Banana', itazame hapa
Majibu ya tathmini yawabeba Giorgio Chielini, Andrea Barzagli

Comments

comments