Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Marco Reus ametemwa katika kikosi cha mwisho cha timu ya taifa ya Ujerumani ambacho kitakwenda nchini Ufaransa kuwania taji la Euro 2016.

Muda mchache uliopita kocha mkuu wa Ujerumani Joachim Low, ametaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 23, na alisababisha mshangao pale alipoliondoa jina la mshambuliaji huyo kwa kutoa sababu za kuwa majeruhi.

Reus alikosa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Slovakia, kutokana na majeraha ya nyama za paja.

Low amesema kabla ya kufanya maamuzi ya kumuacha mshambuliaji huyo, jopo la madaktari wa timu ya taifa ya Ujerumani lilimfinyia vipimo kwa kumpa mazoezi ya kukimbia na imebainika kuna tatizo ambalo litamnyima uhuru kama atacheza kwa kipindi hiki.

“Anaweza kukimbia lakini jereha lake litakua kikwazo kuwa katika sehemu ya timu itakayokua na shughuli ya kupambana wakati wote.” Low aliwaeleza waandishi wa habari.

Hatua hiyo itakua ni bahati mbaya kwa Reus, kwani wakati wa mazoezi ya mwisho kabla ya kutajwa kwa kikosi cha Ujerumani ambacho kilikwenda kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka 2014, aliumia na kusababisha kukosa nafasi ya kuwa kikosini.

Hata hivyo kiungo wa Manchester United, Bsatian Schweinsteiger ametajwa kwenye kikosi cha mwisho japo inaendelea kuripotiwa ana majeraha ambayo yalimfanya ashindwe kumaliza msimu wa 2015-16.

Wachezjai wengine wanne walioachwa kwenye kikosi cha Ujerumani ni Karim Bellarabi, Sebastian Rudy na Julian Brandt.

Kikosi cha mwisho cha Ujerumani ambacho kitakwenda nchini Ufaransa kwa shughuli ya kuusaka ubingwa wa Euro 2016, upande wa walinda mlango yupo Manuel Neuer (Bayern Munich), Bernd Leno (Bayer Leverkusen), Marc-Andre ter-Stegen (Barcelona)

Mabeki: Jerome Boateng (Bayern Munich), Emre Can (Liverpool), Jonas Hector (Koln), Benedikt Howedes (Schalke), Mats Hummels (Borussia Dortmund), Shkodran Mustafi (Valencia), Antonio Rudiger (Roma)

Viungo: Sami Khedira (Juventus), Bastian Schweinsteiger (Manchester United), Mesut Ozil (Arsenal), Andre Schurrle (Wolfsburg), Toni Kroos (Real Madrid), Mario Gotze (Bayern Munich), Julian Draxler(Wolfsburg), Leroy Sane (Schalke), Julian Weigl (Borussia Dortmund), Joshua Kimmich (Bayern Munich)

Washambuliaji: Thomas Muller (Bayern Munich), Mario Gomez (Besiktas), Lukas Podolski (Galatasaray)

NEC Yaiazima NIDA baadhi ya mitambo ya TEHAMA.
Vicente del Bosque Ataja Kikosi Chake Cha Mwisho