Klabu ya Hull City imethibitisha kumpa ajira Marco Silva kama mkuu wa benchi la ufundi, ikiwa ni siku moja baada ya kumtimua Mike Phelan.

Silva, ambaye amewahi kuwa meneja wa klabu za Olympiakos (Ugiriki) na Sporting Lisbon (Ureno), amekubali kusaini mkataba wa kufanya kazi KCOM Stadium hadi mwishoni mwa msimu huu.

Silva amekubali kuchukua nafasi ya kuwa mkuu wa benchi la ufundi klabuni hapo, huku akitambau kazi ngumu iliyo mbele yake ni kuhakikisha anainasua Hull City katika janga la kuburuza mkia wa msimamo wa ligi ya nchini England.

“Marco ni meneja kijana na ametuvutia kutokana na falsafa zake za ufundishaji,” Alisema makamu mwenyekiti wa Hull City Ehab Allam kupitia tovuti na klabu hiyo.

“Amekua na rekodi nzuri katika kazi zake, tunaaminia taweza kufanikisha mikakati ya kutufikisha tunapopataka kwa msimu huu.

“Tupo tayari kumpa ushirikiano wa kutosha, ili kuhakikisha kila tunalolipanga linafanikiwa kutokana na kutambua ushindani unaotukabili katika kipindi hiki ambacho kwetu tunaamini ni cha mpito.”

Marco natarajiwa kuanza kazi ya kukiongoza kikosi cha Hull City mwishoni mwa juma hili katika mchezo wa kombe la FA, ambapo kikosi chake kitakua na shughuli ya kuikabili Swansea City.

Fonte Aomba Kuondoka St Marries Stadium
Arsenal Yapata Majanga, Viungo Wawili Wasalia Kikosi