Kiungo wa klabu bingwa nchini Ufaransa Paris St Germain (PSG) Marco Verratti atakosa sehemu ya msimu wa 2017/18 iliyosalia, kufuatia majeraha ya nyonga yanayomkabili.

PSG wamethibitisha taarifa za kiungo huyo, muda mchache uliopita na atakosa mchezo wa fainali ya kombe la Ufaransa (French Cup) utakaochezwa Mei 08.

“Marco Verratti atafanyiwa upasuaji ambao utamuweka nje hadi msimu ujao wa 2018/19,” imeeleza taarifa za PSG.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, kiungo huyo kutoka nchini Italia ambaye aliwahi kukabiliwa na majeraha ya nyonga siku za nyuma, huenda akaanza kuonekana tena uwanjani wakati wa maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

PSG, ambao tayari wameshajihakikishia kutwaa taji la Ligue 1 msimu huu kutoka kwa wapinzani wao wa karibu AS Monaco, watacheza mchezo wa fainali wa kombe la Ufaransa dhidi ya klabu ya Les Herbiers inayoshiriki ligi daraja la tatu, jumanne juma lijalo.

Bruno Martins Indi kuwasubiri Swansea City
95 wapoteza maisha kwa kimbunga cha vumbi

Comments

comments