Beki kutoka nchini Hispania na klabu ya Chelsea Marcos Alonso amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya mgharibi mwa jijini London.

Alonso mwenye umri wa miaka 27, amekamilisha mpango wa kusaini mkataba mpya, ambao utamuweka Stamford Bridge hadi mwaka 2023, na ni dhahir unavunja tetesi za kuondoka kwake mwishoni mwa msimu huu, ambapo klabu ya Real Madrid ilikua inatajwa kumuwinda.

Beki huyo alijiunga na Chelsea mwaka 2016 akitokea Fiorentina, amekua muhimili mkubwa kwenye kikosi cha The Blues, na tayari ameshafanikiwa kutwaa ubingwa wa England msimu wa 2016/17 pamoja na kombe la chama cha soka nchini humo “FA” msimu uliopita.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha mpango wa kusaini mkataba mpya, Alonso alisema: “Ninajihisi furaha kutokana na tukio hili ambalo linaniwezesha kuendelea kukaa hapa kwa miaka mingine mitano,”

“Nimekua na maisha mazuri tangu nilipojiunga na Chelsea, mazingira ya hapa yamenifurahisha na kunifunza mambo mengi katika soka lengu, ninaamini katika kipindi cha miaka mitano mingine nitakayokua hapa, kuna mengi mazuri yatatokea ili kudumisha furaha niliyonayo hii leo.”

Alonso tayari ameshaifungia Chelsea mabao 15 katika michezo 92 aliyocheza mpaka sasa, na kwa mara ya kwanza aliitwa kwenye kikosi cha wakubwa cha timu ya taifa ya Hispania mwezi March mwaka huu.

Wanakijiji waomba serikali iwapelekee mganga wa jadi
Sadio Mane kurejea kikosini leo